News
Rais Ruto afungua rasmi kituo kipya cha reli cha Miritini kisiwani Mombasa
Rais William Ruto amefungua rasmi kituo kipya cha reli cha Miritini kisiwani Mombasa.
Katika taarifa yake wakati wa uzinduzi huo Rais Ruto alisema abiria watakuwa wakilipa shilingi 50 pekee kutoka mjini Mombasa hadi katika kituo hicho cha reli.
Rais Ruto alisema kituo hicho kitasaidia katika kuimarisha uchukuzi na pia ni sehemu ya juhudi za serikali kuendeleza miundombinu ya reli nchini.
‘’Bei ya kutoka hapa kisiwani Mombasa hadi katika kituo kipya cha reli itakuwa itatoka hiyo shilingi mia tatu kwa matatu, shilingi mia nane kwa teksi mpaka shilingi hamsini’’ alisema Rais Ruto.
Kituo hicho kinatarajiwa kuhudumia takriban watu elfu nne kwa siku na kimegharimu zaidi ya shilingi billioni 6, lengu kuu likiwa ni kusaidia kupunguza msongamano wa magari katika barabara mbalimbali jijini Mombasa.

Rais Ruto anaelezwa mipango ya ujenzi wa kituo cha Reli
Rais Ruto pia alisema mikakati inaendelezwa kuimarisha kaunti za pwani kimaendeleo na bandari ya Mombasa itapanuliwa ili kubuni nafasi mbalimbali za ajira kwa wenyeji.
‘’Nimezungumza na baadhi ya wawekezaji kuhakikisha tunafanikisha miradi ya maendeleo hapa pwani’’ Aliongeza Rais Ruto.
Vilevile, rais Ruto alisema shilingi bilioni 4.6 zimetengwa ili kufaniuisha ujenzi wa barabara mbalimbali katika kaunti ya Mombasa.
Taarifa ya Janet Mumbi