News

Rais Ruto awapongeza maafisa wa Polisi nchini

Published

on

Rais William Ruto ameahidi kuwaunga mkono maafisa wa polisi katika kutekeleza majukumu yao ya kulinda haki za kila mwananchi.

Rais Ruto alisisitiza haja ya kulinda pia Katiba ya Kenya pamoja na kulinda usalama wa Taifa, akisema hatua hiyo itachangia zaidi taifa kushuhudia amani na uzalendo.

Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi siku ya Jumanne tarehe 24 Juni, 2025 Kiongozi wa taifa aliwapongeza maafisa wa polisi wakiongozwa na Inspecta Jenerali wa Polisi nchini Douglas Kanja akisema wamejitolea kuhakikisha taifa la Kenya linaishi kwa Amani.

Rais Ruto alisema viongozi wanaojaribu kuwatishia maafisa wa polisi wanapotekeleza shughuli zao hawawezi kudhalilisha kitengo cha polisi mbele ya macho yake.

“Kuna viongozi wengine wenye kukejeli maafisa wa polisi wanapotekeleza majukumu yao, hiyo haifai tuwape nafasi polisi wetu waendeleza kazi zao kwa kuzingatia sheria na kulinda wananchi bila ya kusumbuana kwa sababu Kenya ni yetu sisi sote”, alisema Rais.

Vile vile alipongeza juhudi za maafisa wa usalama kutoka nchini Kenya ambao wao nchini Haiti katika katika oparesheni ya Kiusalama kama njia moja wapo ya kuleta Amani nchini humo.

Picha kwa hisani

Kwa upande wake Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Douglas Kanja, aliahidi kwamba maafisa wa polisi watatekeleza majukumu kwa kuzingatia sheria na mwongozi wa Katiba.

Haya yanajiri huku Wanaharakati wa kutetea haki za kibinaadamu pamoja na vijana wa kizazi cha Gen-z wakishiriki maandamano ya kupinga ukatili unaotekelezwa na maafisa wa polisi nchini.

Hata Juni 25 siku ya Jumatano, vijana wa Gen Z walidai kwamba watashiriki maandamano ya amani kushinikiza kuwajibika zaidi sawa na kuchukuliwa hatua kwa maafisa wa polisi wanaohusika na mauaji ya wananchi kiholela.

Taarifa ya Elizabeth Mwende

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version