News
Sarai, amkosoa Waziri Murkomen kwa madai ya kuhujumu mashirika ya kiislamu
Katibu mkuu wa Chama cha UDA Hassan Omar Sarai, imemkosoa Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen kutokana na kuchapisha katika gazeti rasmi la serikali kundi cha Muslim Brotherhood na Hizb-ur-Tahrir kama mashirika la kigaidi.
Sarai alisema hatua hiyo inahujumu jamii ya Waislamu nchini na hata katika mataifa ya ughaibuni, akisema ingekuwa bora zaidi iwapo serikali ingechapisha katika gazeti hilo kundi la Zionist la Israel kama Shirika la Kigaidi.
Sarai alipendekeza kufanyiwa marekebisho kwa sera za kimataifa za Kenya na kutoa wito wa kuwepo kwa uwiano thabiti na jamii ya kiislamu ulimwenguni huku akipinga uhusiano na taifa la Israel.
Wakati huo huo alisema Waziri Murkomen alitumia sera ya kudhibiti ugaidi ya mwaka wa 2025 kukandamiza mashirika hayo, na hivyo basi ni yeye pekee ndio mwenye uwezo ama Mahakama ya Kenya kuondoa chapisho hilo kwenye gazeti rasmi la serikali.
Hata hivyo alidokeza kwamba suala hilo limeangaziwa katika mataifa mbalimbali na huenda likachangia athari kubwa ya kiusalama kutokana na kuhusishwa kwa itakadi na vurugu.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi