News
Serikali yasema vitambilisho elfu 400 havijachukuliwa kwa ofisi za umma
Serikali imetangaza kwamba zaidi ya Vitambulisho vya kitaifa elfu 400 kote nchini havijachukuliwa na wenyewe licha ya kutuma maombi ya kutafuta stakabadhi hiyo muhimu ya kitaifa.
Katibu katika Idara ya uhamiaji nchini Belio Kipsang, alisema licha ya maafisa wa umma kuhakikisha wanawataka wakenya ambao hawajachukua Vitambulisho vyao vya kitaifa bado kuna changamoto za kuwafikia watu hao.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kushiriki zoezi la upinzi wa miti katika siku ya Mazingira nchini, Kipsang aliwahimiza wakenya ambao bado hawajachukua Vitambulisho vyao vya kitaifa kutembelea ofisi husika na kuchukua stakabadhi hiyo.
Katibu huyo wa idara ya uhamiaji nchini, alisema changamoto hiyo imesababisha zoezi endelevu la usajili wa wapiga kura inaloendelezwa na Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kushuhudia idadi ndogo ya wakenya wanaojitokeza kusajiliwa.
Wakati huo huo alidokeza kwamba serikali itashirikiana na maafisa tawala ikiwemo machifu kuhakikisha vitambulisho hivyo vya kitaifa vinawafikia wenyewe bila changamoto.