News
Serikali yaweka wazi hatua ilizopiga chini ya uongozi wa Rais Ruto
Serikali imeweka wazi hatua ilizopiga katika kipindi cha miaka mitatu tangu Rais William Ruto achukue hatumu ya uongozi nchini.
Katika taarifa iliyotolewa na taifa kupitia vyombo vya habari na Msemaji wa serikali Isaac Mwaura, imeguasia baadhi ya vipengele vilivyoangaziwa na serikali katika kipindi cha miaka mitatu ambapo serikali imeonyesha mafanikio yake.
Katika sekta ya Utalii, serikali imesema utalii unakuwa kwa kasi kwani watalii wa kimataifa wanaowasili wakifikia milioni 2.42 na mapato kutoka kwa sekta hiyo kufikia shilingi bilioni 462.21.
Mwaura ameeleza kwamba ukuaji huu unadhihirisha juhudi za serikali katika kufufua utalii na kuhifadhi wa Wanyamapori na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa na kuongeza ajira katika sekta hiyo.
Akigusia ukuaji wa uchumi wa taifa, Mwaura ameweka wazi kwamba serikali ina dhamira ya kuendeleza juhudi hizo chini ya mpango wa ajenda ya mabadiliko ya kiuchumi yaani Bottom up Economy Transformation Agenda {BETA}, akisema umechangia ajira kwa vijana, utoaji wa huduma, na uwezeshaji wa kiuchumi.
Wakati huo huo alifafanua kwamba huduma za afaya nchini zinaendelea kuwafikia wananchi mashinani, kwani wakenya milioni 25.8 tayari wamejisajili na Mamlaka ya afya ya jamii SHA kwnai zaidi ya wasimamizi wa afya ya jamii laki moja wamepokea mafunzo ya kutoa huduma mashinani.
Aidha kwenye sekta hiyo ya Afya, zaidi ya hospitali 350 zimejenhwa na kupandishwa vyeo huku vituo vya afya 10,582 vikiwekwa kwenye mfumo wa kidijitali ili kuimarisha utoaji wa huduma ikiwemo Saratani, magonjwa sugu miongoni mwa mengine.
Hata hivyo kwenye sekta ya Kilimo, serikali imepiga hatua kubwa katika kufufua kilimo hatua iliyosababisha kushuka kwa bei ya unga wa Mahindi kwa asilimia 34 na kuboresha upatikanaji wa chakula na zaidi ya wakulima milioni 7 wakisajiliwa katika hifadhi data ya kidijitali na mifuko milioni 21 ya mbolea imesambazwa nchini.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi