News
Takriban vijana wahalifu 500 wamekamatwa Malindi
Idara ya usalama mjini Malindi katika kaunti ya Kilifi imesema itaendelea kutekeleza oparesheni ya kuwasaka wahalifu wanaoendelea kuhangaisha wakaazi.
Mafisa waa usalama walisema kufikia sasa takriban vijana 500 wanaohusishwa na visa vya wizi wa kimabavu wamekamatwa.
Kulingana na naibu kamishna David Lusava, katika siku za hivi karibuni eneo hilo limeshuhudia utovu wa usalama akitaja eneo la Kwachocha, Shela, Mtangani, Maweni miongoni mwa sehemu nyengini mjini humo.
Lusava alihakikishia wakaazi eneo hilo kuwa vyombo vya usalama vimejitolea kuhakikisha usalama unadumishwa.
“Malindi kwa mda kumekuwa na utovu usalama lakini tumejaribu kudhibiti vijana wengi ambao wamekuwa wakihangaisha watu, lakini kwa sasa wengi wamekamatwa na wamefikishwa mahakamani, Kwa sasa wale wamekamatwa ni karibu vijana 500 na hii oparesheni tumeifanya ndani ya mda wa mwezi mmoja.
Wakaazi katika maeneo hayo wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa usalama kutokana na uvamizi unaotekelezwa na magenge ya uhalifu yanayopora mali na kujeruhi wakaazi hao.
Miongoni mwa magenge yanayotajwa kuhangaisha wakaazi ni kundi la vijana wanaojiita “Mawoza” ambapo idara ya usalama imeahidi kukabiliana nalo
Taarifa ya Joseph Jira