News

Uhaba wa maji wakera wakaazi Mombasa

Published

on

Wakaazi wa mtaa wa mabanda wa Bangladeshi eneo bunge la Jomvu, kaunti    ya Mombasa, wanalalamikia uhaba mkubwa wa maji unaoendelea kushuhudiwa kwa zaidi ya mda wa wiki tatu sasa.

Wakiongozwa na Betty Achieng’, wakaazi hao walisema hali hiyo imeathiri pakubwa shughuli zao za kila siku.

Walisema bei ya maji imeongezeka mara dufu kutokana na uhaba huo.

Aidha walisema wanalazimika kununua maji kutoka kwa wauzaji wa rejareja, wanaotumia mikokoteni huku wakihofia usalama wa maji hayo, hasa katika matumizi ya nyumbani.

“Tunaomba msaada kwa serikali itusaidie kwa mambo ya maji, angalia vile tunahangaika hata kazini hatuendi kwa sababu vitu vyetu ni vichafu, tuko na watoto wadogo, nguo ni chafu, saa zingine tunakaa hapa tunakaa hapa tunangoja msaada wa maji”, walisema wakaazi hao

Kwa upande wao, maafisa kutoka wizara ya maji ya kaunti ya Mombasa walieleza kuwa tatizo hilo linatokana na upungufu wa maji katika kituo cha kusambaza maji cha Baricho kaunti ya Kilifi, hali iliyosababisha maeneo mengi ya kaunti hiyo kukosa bidhaa hiyo muhimu.

Taarifa ya Mwanahabari wetu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version