News

Viongozi wa dini wamkosoa Kithure Kindiki.

Published

on

Viongozi wa dini ukanda wa wamemkosoa naibu rais profesa Kithure Kindiki kuhusiana na kauli yake kwamba baadhi ya viongozi wa dini na wanadiplomasia walihusika katika kuunga mkono maandamano ya vijana wa kizazi cha Gen Z ya mwezi juni 25 2025.

Mwenyekiti wa kitaifa wa baraza la kuu la waislamu SUPKEM Sheik Muhdhar Khitamy alisema matamshi ya Kindiki ni siasa zinazolenga kuwanyooshea lawama viongozi wengine.

Sheikh Kitamy alisema kuwa kwa sasa wanasiasa wamekuwa na usemi mkubwa kutokana na hulka ya kuwahonga wananchi na kuwafanya viongozi wa dini kutosikizwa.

Akizungumza na wanahabari kiongozi huyo wa dini ya kiislamu alionya kuwa  iwapo wakenya hawatakuwa makini, kunauwezekano wa taifa kuelekea pabaya kutokana na vijana kutumiwa vibaya na wanasiasa.

“Ukweli wa mambo ni kwamba wanasiasa wanachukuwa jukumu kubwa sana kwa sababu ya pesa za kuwatumia watu, jambo lolote liwe la kikatiba au nini utaona linawahusisha hao wanasiasa, twawaambia wanasiasa hao ndio chumvi, watengeneze nchi, watakuja kujuta kwasababu hali inavyokwenda ni mbaya”, alisema Khitamy.

Naye mwakilishi wa vijana katika baraza hilo Abdhulmalik Ali aliwataka vijana nchini kuwa makini na kufuata ushauri wa kisheria iwapo hawajaridhishwa na utendakazi wa viongozi.

Ali vile vile aliwashinikiza vijana kuepuka maandamano ya vurugu.

“Wanasiasa tuchungane nao, niwatu wanamaslahi yao zaidi ya wewe kijana, hii kenya inakuhitaji wewe kijana, kama kiongozi anatufaa tumpigie kura muhula ujao, kama hatufai njia iko ya kumtoa lakini sio suala la kumwaga damu”, alisema Abdhulmalik.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version