Business

Wafanyabiashara wa Korosho walalamikia kupanda kwa bei ya mafuta.

Published

on

Wafanyabiashara wa korosho katika soko la Oloetiptip mjini Kilifi kaunti ya Kilifi wanairai serikali kushughulikia suala la kupanda kwa bei ya mafuta.

Kulingana na wafanyibiashara hao wanasafirisha korosho kutoka kaunti ya Lamu hali na ni ghali sana.

Wakizungumza na mwanahabari wetu wafanyibiashara hao waliongeza kuwa gharama  ya usafirishaji imepanda kutokana na ongezeko la mafuta hali inayowapelekea kukadiria hasara.

Aidha wanasema bei ya korosho kwa  sasa imepanda kwa shilingi 130 ambapo pia wanasema itawalazimu kuongeza 200 ili wauze shilingi  1700 kwa kilo .

Wafanyibiashara hao  wamesema kuwa  imewalazimu kupandisha bei na hata kupunguza kiwango ili wapate faida ndogo kujikimu kimaisha.

Wameitaka serikali kuangazia upya swala la kupanda kwa gharama ya  mafuta ili kuwapunguzia hasara ambazo wanakadiria kwa sasa.

Wanasema eneo hili halina korosho kwa sasa zile zinaapatika ziko ghali huku wakiwataka wakulima kukumbatia kilimo cha kisasa ili kuongeza zao hilo.

“ Tunatoa korosho kutoka kaunti ya lamu na kutoka huko hadi huku nauli iko juu hali ambayo inatufanya tukiuza hatupati faida , na sai ambapo mafuta yamepanda bei nauli pia imepanda pia korosho zenyewe ziko ghali hali inayofanya biashara kuwa ngumu.

”Tunaiomba serikali inaangalie wafanyibiashara kwanu tunaumia sana.”

Taarifa ya Pauline Mwango

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version