News
Wahadhiri waanza mgomo wa kitaifa
Muungano wa Wahadhiri wa vyuo vikuu nchini (UASU) wameanza mgomo wao licha ya Hazina ya kiaifa kutoa shilongi bilioni 2.5 kwa ajili ya kutekeleza awamu ya pili ya mkataba wa makibaliano wa CBA wa 2021-2025.
Wahadhiri hao walisitisha kazi zao Jumatano Septemba 17, 2025 wakidai kuwa madai yao ya kifedha bado hayajatimizwa kama walivyokubaliana serikali.
Katibu wa UASU tawi la Nairobi, Dkt. Maloba Wekesa, alisema serikali imeshindwa kutimiza ahadi yake, akisisitiza kwamba wahadhiri wataendelea na mgomo.
Alibainisha kwamba shilingi bilioni 7.9 za malimbikizo chini ya CBA ya mwaka 2017 bado hazijalipwa licha ya Mahakama kuu mwenzio Machi mwaka 2025 kuagiza suala hilo kutekelezwa kikamilifu.
Wekesa alidai kwamba wafanyakazi wamesalia kama ombaomba wakati ambapo awamu ya pili ya malipo yao ilipaswa kulipwa licha yao kuipa serikali muda wa siku 7 kutekeleza ahadi yao baada ya kuichelewesha kwa muda wa miezi 3.
“Katika 2017-2021 tulikuwa na CBA sawa. Iliichukua serikali miezi 36 kuandika makubaliano. Tulinyimwa nyongeza ya kila mwaka. Mahakama zikaamuru utekelezaji. Tarehe 25 Machi 2025, mahakama ikaamua kwa upande wetu”, alisema Wekesa.
Aliongeza kuwa serikali ilikuwa imeahidi kutekeleza kikamilifu CBA ila kumekuwa na kimya tangu hapo huku akiongeza kuwa masuala ya afya ya wahadhiri wa UoN hayakuchukuliwa kwa uzito ilhali uongozi ulipaswa kushughulikia masuala hayo muhimu.
Kwa upande wake Katibu wa tawi la Nairobi wa Chama cha Wafanyakazi wa vyuo vikuu (KUSU), Peter Waita, aliongeza kuwa wahadhiri wamenyimwa haki yao ya msingi.
Taarifa ya Elizabeth Mwende