Business
Wahudumu wa Tuktuk walalamikia kupanda kwa bei ya mafuta
Wahudumu wa sekta ya uchukuzi wa Tuktuk katika wadi ya Mariakani eneo la bunge la Kaloleni kaunti ya Kilifi wanaendelea kulalamikia gharama ya juu ya bei ya mafuta ya petroli hali ambayo imeathiri biashara zao.
Kulingana na baadhi ya wahudumu hao, bidhaa zisizo na msingi zimeshuka bei ilhali bei ya mafuta ikionekana kuendelea kupanda jambo ambalo walisema imekuwa changamoyo wa wahubumu wengi.
Wakizungumza na Coco Fm , wahudumu hao wa Tuktuk walidai kwamba tangu kuongezwa kwa bei ya mafuta ya Petroli kwa shilingi nane wengi wao wamepata changamoto hata zaidi huku wakipoteza wateja baada ya kujaribu kuongeza nauli kwa wateja wao.
Hata hivyo, waliitaka serikali kuu kuingilia kati swala hilo mara moja kwani asilimia kubwa ya wahudumu hao wanaendelea kupata hasara.
Wakati huo huo walipendakaza bidhaa ambazo sio muhimu kama vile sigara na Pombe kuongezwa bei na na kupunguza bei za mafuta na vyakula.
Taarifa ya Pauline Mwango