News
Wahuni watatiza maandamano ya vijana Nairobi
Maandamano ya vijana wa Gen Z jijini Nairobi wanaoshinikiza Naibu Inspekta jenerali wa polisi Eliud Lagat kujiuzulu yalikumbwa na changamoto baada kundi la vijana wahuni kuingilia kati na kuyatatiza.
Waandamanaji hao walilazimika kukimbilia usalama wao wakati magenge ya vijana waliokuwa kwenye bodaboda walipowakabili.
Wahuni hao walifika kwa kishindo wakiwa kwenye pikipiki kadhaa na kuwazuia vijana waliokuwa wakiandamana kwa amani kuelekea kituo kikuu cha polisi kwenye makutano ya University Way.
Waandamanaji waliwacha kambi pinzani kuchukua udhibiti na kutawala huku wakiondoka na kuwachapa viboko waliosalia barabarani.
Magari ya polisi na maafisa wa usalama walionekana wakishuhudia jinsi magenge hayo yalivyokuwa yakiwakimbiza na kuwafanyia fujo waandamanaji.
Hapo awali, polisi walikuwa wametumia vitoa machozi kutawanya umati uliokuwa umekusanyika katika kituo cha Nation ambapo ghadhabu ilianza.
Mvutano huo ulilemaza shughuli za biashara ndani ya jiji la Nairobi na maduka kufungwa huku Waandamanaji hao wakifanikiwa kutekeleza pikipiki ya wahuni hao.
Lagat alitangaza kujiuzuli kwa mda siku ya Jumatatu 16, Juni 2025 kufuatia shinikizo za vijana, wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na viongozi wa kisiasa baada ya kuhusishwa na kifo cha mwanablogu Albert Ojwang.
Taarifa ya Joseph Jira