News

Wakaazi wa Chumani wafunga barabara kuu ya Malindi-Mombasa

Published

on

Wakaazi wa eneo la Chumani, Wadi ya Matsangoni Kaunti ya Kilifi, wameandamana kulalamikia kucheleweshwa kwa ujenzi wa barabara ya Malindi-Mombasa, wakidai kwamba barabara hiyo imekuwa hatari kwa usalama wa watumiaji wa barabara hiyo kutokana na kuongezeka kwa visa vya ajali hasa katika eneo hilo la Chumani.

Wakingozwa na Mwenyekiti wa Chama na waendeshaji Boda boda eneo la Chumani Eric Kenga, mamia ya wakaazi hao waliziba barabara katika kituo cha mabasi cha Chumani na kutatiza usafiri katika barabara hiyo ambayo kwa kawaida huwa yenye shughuli nyingi.

Maandamano hayo yanafanyika siku chache tu baada ya basi moja la shule lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi kubingiria karibu na shule ya Upili ya Chumani.

Hakuna mwanafunzi aliyefariki wakati wa ajali hiyo ila majeruhiwa walipelekwa Hospitali kwa matibabu kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Waandamanaji hao walisema barabara hiyo imejaa mashimo na sasa wanaitaka serikali kupitia kwa Halmashauri ya barabara kuu nchini (KeNHA) iwajibike.

Mwakilishi wadi wa eneo la Matsangoni Hassan Mohammed ambaye pia alishiriki Maandamano hayo alisema atawaongoza wakaazi wa sehemu hiyo kuandamana na kufunga barabara hadi hali hiyo itakaporekebishika.

Taarifa ya Eric Ponda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version