News

Wakaazi wahimizwa kushirikiana na asasi za kiusalama

Published

on

Naibu Chifu wa Shella mjini Malindi kaunti ya Kilifi Nicodemus Mwayele ametoa wito kwa wenyeji kushirikiana na asasi za usalama ili kuyakabili magenge ya kihalifu ambayo yanazidi kutekeleza visa vya uhalifu maeneo mbalimbali ya mji huo.

Akizungumzia katika kikao cha umma cha kutoa maoni kuhusu namna ya kuyakabili magenge hayo, ambacho kiliandaliwa eneo la Muyeye ,Pentagon na kuwaleta pamoja Maafisa tawala, Wanaharakati na Wananchi, Mwayele alisema magenge hayo yanazidi kuchipuka hali ambayo inaendelea kuwatia hofu Wananchi.

Mwayele alisema watoto wengi eneo hilo hawaendi Shule kutokana na utumizi wa dawa za kulevya.

Kwa upande wa baadhi ya Wananchi walilalamikia hali ya Wazazi kuzembea katika malezi ya watoto wao huku wengine wakiinyoshea Idara ya usalama kidole cha lawama wakidai imetepetea katika kukabiliana na wahalifu mjini Malindi.

Wakaazi wa Shella mjini Malindi kaunti ya Kilifi wahudhuria vikao vya kukusanya maoni ya umma kuhusu usalama

Nao baadhi ya wanaharakati wakiongozwa na Victor Kaudo na Famau Mohamed Famau walidai kwamba Kituo cha kupeana dawa aina ya Methadone katika hospitali ya Kaunti ndogo ya Malindi kinachangia Kwa ongezeko la Vijana wanaotumia dawa za kulevya.

Vilevile, waliitaka oparesheni ya kuwarudisha watoto shuleni kurejeshwa kwani Idadi kubwa ya watoto hawaendi shuleni.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version