Sports
Bado Hawajamaliza Kulipa Starlets Asema Rais Wa FKF
Rais wa Shirikisho la mchezo wa soka nchini Hussein Mohammed amefichua kwamba wamelipa badhi ya marupurupu kwa kikosi cha soka kwa akina dada Harambee Starlets.
Hata hivyo akizungumza na kituo kimoja nchini Mohammed amefichua kwamba bado hawajalipa marurupu ya kikosi hicho mechi za kirafiki dhidi ya Ivory Coast mwezi April,Rais huyo akiongezea kwamba kazi ya kulipa wachezaji hao ni ya Serikali kupitia wizara ya michezo na wala si ya Shirikisho la soka nchini.
“Tumelipa badhi ya marupurupu kulikuwepo na tatizo upande wa wizara ila swala hilo sasa limetatuliwa akina dada hao watapokea pesa zao ikiwemo ya Cecafa nchini Tanzania.”
Alipoulizwa iwapo kama ndiyo chanzo ya badhi ya wachezaji kujiondoa kwenye kambi ya Starlets Hussein amesema wanasubiri ripoti kutoka kwa kocha wa timu hiyo Beldine Odemba.
Starlets wako nchini Tanzania mashindano Afrika Mashariki na kati CECAFA.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

