Sports
Botswana yatangaza siku ya Mapumziko Septemba 29 kusherehekea dhahabu ya Tokyo
Rais wa Botswana Duma Boko ametangaza Septemba 29 mwaka huu kuwa siku ya mapumziko kusherehekea ushindi wa dhahabu ya Dunia na timu ya wanariadha wanne kupokezana kijiti kwa wanaume.
Timu hiyo iliandikisha historia katika mashindano ya Riadha Ulimwenguni iliponyakua dhahabu hiyo katika siku ya mwisho jana Jumapili, ikiwa mara ya kwanza taifa la Afrika kutawazwa mabingwa katika fainali hiyo.
Kikosi cha Botswana katika fainali hiyo kiliwashirikisha bingwa wa Olimpiki katika mita 200 Letsile Tebogho, bingwa wa dunia wa mita 400 Collen Kibinatshipi na Bayapo Ndori.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

