Sports
Chelsea Yathibitisha Kunasa Joao Pedro
Kilabu ya Chelsea imethibitisha kumsajili mshambulizi wa kilabu ya Brighton and Hove Albion FC Joao Pedro raia wa Brazil kwa pauni milioni 60.
Mchezaji huyo amesafiri tayari Marekani baada ya kukamilisha vipimo vya kimatibabu mjini london NA kutia wino mkataba wa miaka mitano na The Blues.
Nyota huyo anakua sajili wa tatu kwa Chelsea ambao mpaka sasa wametumia zaidi ya pauni milioni 200 katika kusajili wachezaji.
Pedro mwenye umri wa miaka 23 sasa yuko njia nyeupe kuwakilisha The Blues kwenye mechi ya robo fainali Kombe la Dunia baina ya vilabu nchini Marekani dhidi ya Fluminese ya Brazil.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

