Sports
Chipukizi wa Kenya Rising Starlets waanza safari ya kufuzu Kombe la Dunia la FIFA U-20 mwaka 2026, huku Kocha Mkuu Jackline Juma akilenga kujenga kikosi thabiti kwa kampeni hiyo.
Mkufunzi wa kikosi chipukizi akina dada Jackline Juma amefichua kuwa kikosi cha muda kilichotangazwa kina mchanganyiko wa vipaji vipya vinavyoibukia na wachezaji wenye uzoefu. Baada ya kupita raundi ya kwanza bila kucheza, Kenya itakutana na Ethiopia katika raundi ya pili ya kufuzu.
Mchuano wa mikondo miwili utaanza nchini Ethiopia kati ya Septemba 19 na 21, kisha kurejea jijini Nairobi kwa mechi muhimu ya marudiano, iliyopangwa kuchezwa kati ya Septemba 26 na 28.
Mshindi atafuzu kuingia raundi ya tatu, ambapo atakabiliana na mshindi wa kati ya Tanzania au Angola mnamo Februari 2026.
Mchakato muhimu wa uteuzi umetiliwa mkazo, kwa kambi mbili ndogo za mazoezi zilizoundwa kusaidia benchi la ufundi kupunguza orodha ya wachezaji wa awali hadi kikosi cha mwisho. Kikundi cha kwanza cha wachezaji tayari kimeripoti kambini, huku kundi la pili la wachezaji 30 likitarajiwa kujiunga mwishoni mwa wiki hii.
Kutoka kwa makundi haya, Kocha Juma na benchi lake la kiufundi watawapima wachezaji kwa ubora wa kifiziki na kimbinu kabla ya kutaja kikosi cha mwisho kitakachokabiliana na Ethiopia.
Kocha Juma analenga wachezaji wenye uzoefu kutoka Kenya Women Premier League (KWPL) na Kenya National Super League (NSL).
Baadhi ya wachezaji walioshiriki Kombe la Dunia la U-17 mwaka 2024 wamepanda ngazi hadi kikosi cha U20, na huenda wakajumuishwa katika kikosi cha Juma.
“Tunahitaji kuchanganya wachezaji wenye uzoefu kama Fasila na wale wa U-17 ili kupata kikosi imara kitakachotupa matokeo tunayoyataka,” alisema Juma.
Wachezaji kadhaa waliowahi kushiriki Kombe la Dunia la Wanawake U-17 huko Dominican Republic wamepandishwa daraja, akiwemo Scovia Awuor, Velma Abwire, Ephy Awuor, Lorine Ilavonga, Rebecca Odato, Halima Imbachi, Marion Serenge, Valarie Nekesa, Elizabeth Ochaka na Lornah Faith.
Fasila Adhiambo na Elizabeth Mideva, ambao pia wameonekana waking’ara hata na kikosi cha wakubwa, wanatarajiwa kuwa uti wa mgongo wa timu.
Kwa kuwa na uzoefu wa kimataifa na ule wa klabu, wachezaji hawa watakuwa muhimu katika kuwaongoza vijana wenzao kwenye mtihani mgumu wa kufuzu kwa bara.
Kikosi cha awali, ambacho kimejumuisha idadi kubwa ya wachezaji wapya kutoka timu mbalimbali, kinaundwa na Mercy Onyango (Wadadia), Judith Okumu (Buruburu Soccer), Florence Kalekye (Kangundo Starlets), Mercy Akoth (Vihiga Queens) na Molvine Owuor (Kayole Starlets), miongoni mwa wengine.
Kadiri chipukizi hawa wa Kenya wanavyojiandaa kukabiliana na timu ngumu ya Ethiopia, kwa maandalizi yenye mpangilio na kikosi chenye usawa, Rising Starlets wameazimia kuthibitisha kuwa wanastahili kuwa miongoni mwa wakali wa Afrika.
“Tunatazamia kushinda mechi na kufuzu kwa Kombe la Dunia,” alisema Jerrine Adhiambo, mchezaji wa Mathare United Women.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

