Sports
India Yakabiliwa na Hatari ya Kusimamishwa na FIFA kwa Mara ya Pili Ndani ya Miaka Mitatu
Taifa la India yaweza kupigwa marufuku kushiriki soka la dunia kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu baada ya FIFA na shirikisho la soka bara la Asia kudai utekelezaji wa katiba mpya kufikia Oktoba 30, la sivyo likabiliwe na adhabu ya kusimamishwa.
Shirikisho la kimataifa la soka (FIFA) na Shirikisho la Soka la Asia (AFC) walituma barua ya pamoja kwa rais wa Shirikisho la Soka la India (AIFF), Kalyan Chaubey, wakieleza “wasiwasi mkubwa” kuhusu kushindwa kuhitimisha na kupitisha katiba hiyo.
“Kukosa kutimiza tarehe hii kutatuacha bila njia nyingine ila kupeleka suala hili kwa chombo husika cha maamuzi cha FIFA ili kizingatiwe na kuamuliwa,” ilisomeka barua hiyo iliyoonekana na AFP. Katiba ya AIFF imekuwa ikisubiri uamuzi katika Mahakama Kuu ya India tangu mwaka 2017.
Kusimamishwa huko kungemaanisha timu za taifa za India na vilabu vyake kupigwa marufuku kushiriki mashindano yote ya kimataifa.
FIFA iliwahi kuisimamisha India mnamo Agosti 2022 kwa kuingiliwa na watu wa tatu baada ya Mahakama Kuu kuunda kamati ya wasimamizi kuendesha AIFF.
Marufuku hiyo iliondolewa siku chache baadaye, jambo lililoruhusu AIFF kumchagua Chaubey kuwa rais.
Kwa sasa, soka la ngazi ya juu nchini India limevurugika.
Ligi kuu ya India (Indian Super League – ISL) inaweza kusambaratika kutokana na mzozo kati ya AIFF na mshirika wake wa kibiashara.
Msimu wa ligi hiyo umecheleweshwa kuanza, na maelfu ya wachezaji na wafanyakazi wako hatarini kupoteza ajira zao.
Mkataba wa haki kati ya AIFF na kampuni inayoendesha ISL, Football Sports Development Limited, unamalizika Desemba 8 na bado haujahuishwa.
AIFF imeshindwa kuwasilisha mpango wa kufufua ISL, ambayo kawaida huchezwa kati ya Septemba na Aprili.
Chama cha wachezaji FIFPRO Asia/Oceania wiki iliyopita kiliwasilisha suala hili kwa FIFA.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

