Sports
Kasarani Njia Nyeupe Mechi Za CHAN
Waziri wa Michezo Salim Mvurya ameweza kukabidhi rasmi uwanja wa Kasarani kwa kamati andalizi ya mashindano ya CHAN ikiwa inashiriria kwamba uwanja huo uko tayari kwa kipute hicho kinachongoa nanga augosti 2 katika mataifa ya Kenya Uganda na Tanzania.
Mechi zote za Harambee Stars dhidi ya DR Congo,Angola,Zambia na Morocco zote zitapigwa katika uga huo ambao umekarabatiwa upya kwa miundo msingi wa kisasa.
vile vile fainali ya kipute hicho kitapigwa katika uga wa Kasarani Agosti 30.
Huku uga wa Benjamin Mkapakatika Tiafa la Tanzania likaanda mechi ya ufunguzi wa Mashindano hayo Agosti 3.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

