Sports
KCB WASHINDA TAJI LA DALA SEVENS 2025 BAADA YA KUWAZIDI NGUVU KABRAS RFC
Kilabu ya KCB wametawazwa mabingwa wa Dala Sevens 2025 baada ya kuwashinda mahasimu wao wakuu Kabras RFC kwa alama 12-7 kwenye fainali ya kusisimua iliyochezwa chini ya mvua katika Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Kisumu.
Wabenki hao tayari walikuwa wamehakikisha kutwaa taji la jumla la National Sevens Circuit mapema siku hiyo baada ya ushindi wa kishujaa wa 15-14 kwenye robo fainali dhidi ya wapinzani wao wakuu Strathmore Leos waliokuwa wakifukuzia ubingwa.
Katika mchezo huo, Vincent Onyala alifungua ukurasa wa alama kwa kukimbia kando na kufunga, ingawa Emmanuel Opondo alikosa kubadilisha. Strathmore walijibu kupitia Brian Mwendwa aliyedanganya ulinzi wa KCB na kufunga chini ya post, huku Arnold Mwita akiongeza alama za ziada na kuwapa Strathmore uongozi wa 7-5 kabla ya mapumziko.
Kabras walitumia fursa baada ya Stephen Osumba kutumwa sin bin na kufunga try isiyobadilishwa, hali iliyosababisha matokeo kuwa 7-5 hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilibaki na ushindani mkubwa, lakini Floyd Wabwire alipata mwanya na kufunga try pekee ya kipindi hicho.
Kabras walijaribu kusawazisha mwishoni, lakini ulinzi wa KCB ulidumu imara na kuwaletea ushindi wa 12-7 na taji la Dala Sevens.
Kocha mkuu wa KCB, Andrew Amonde, alisifu wachezaji wake kwa uthabiti wao, akisema kuwa hiyo ndiyo imekuwa msingi wa ubabe wao msimu huu.
“Uthabiti wetu umekuwa nguzo kuu na hatimaye umetuletea matunda. Ni jitihada za pamoja na tunatumai matokeo haya yataakisiwa pia kwenye mchezo wa 15s,” alisema Amonde baada ya filimbi ya mwisho.
Katika mechi nyingine:
-
Daystar Falcons waliwacharaza Menengai Oilers 31-0 na kumaliza katika nafasi ya tatu.
-
Nakuru RFC waliwazidi nguvu Mwamba RFC 17-10 katika fainali ya nafasi ya tano.
-
Catholic Monks waliwapiga Impala RFC 26-7 kushinda Challenger Cup, huku MMUST wakiwazidi Kisumu 31-0 katika mchezo wa nafasi ya 13.
-
Katika Divisheni ya Pili, Zetech Oaks waliibuka mabingwa baada ya kuwazidi Makueni Ravens 24-12 katika fainali.
Kwa ushindi huo Kisumu, KCB hawakutwaa tu taji la Dala Sevens bali pia wamedhihirisha hadhi yao kama wafalme halisi wa rugby ya sevens nchini Kenya.
Wabenki sasa wanajivunia rekodi ya mataji matano ya National Sevens Circuit, wakijitenga na wapinzani waliobaki ambao wamekwama kwenye mataji manne.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

