Sports
Kikosi Cha Raga Simbas Yashinda Tena
Kikosi cha Raga wachezaji 15 kila upande Simbas imepata ushindi wake wa pili katika mechi za kujipima nguvu kabila ya kombe la bara Afrika baadaye mwakani.
Simbas waliwatandika Super Babarians alama 27-22 mechi iliopigwa mjini Lumpopo Afrika Kusini.
Vijana hao wa kocha Jerome Parwater walikua wametoka sare mechi mbili 17-17 dhidi ya SWD Eagles na vilevile kupteza mechi mbili dhidi ya Chipukizi wa Afrika Kusini Blitz Bocks na Sanlam Bolam.
Timu hiyo imesalia na mechi moja ya kirafiki dhidi ya Limpompo kabila ya mashindano ya kombe la Bara Afrika mjini Kampala Uganda mwezi Julai mechi hizo zikitumika pia kama mechi za kombe la dunia nchini Australia mwaka 2027.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

