Sports
Mancity Inamnyemelea Kiungo Tijjani Reijnders
Kilabu ya Manchseter City iko kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na kiungo wa AC Milani Tijjani Reijnders kumleta ugani Etihad msimu ujao.
Mawakala wa mchezaji huyo wanataka kitita cha pauni milioni 60 kumwachilia mholanzi huyo ambaye amefunga magoli 19 katika mechi 104 ambazo amechezea Milan
Hata hivyo city wako tayari kutoa pauni milioni 55 kupata sahihi yake na kumpa kandarasi nono mkataba wa miaka mitano ugani Etihad.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Milan msimu jana akitokea AZ Alkamar ya Eredivise.
City wangali sokoni kupata mrithi wa kiungo mbunifu Kevin De Bruyne ambaye ameondoka kwenye kilabu hiyo baada ya mafanikio makubwa ikidaiwa pia wanamfukuzia kiungo wa Lyon Ryan Cherki raia wa Ufaransa.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

