Sports
Mariakani FC ya Kaloleni ndiyo mabingwa wa Makala ya kwanza Cocofm Supercup
MARIAKANI FC MABINGWA
Timu ya soka ya vijana ya Mariakani fc ni Moja wapo ya timu zinazo kua Kwa kasi sana kutoka wadi ya Kaloleni, Kaunti ndogo ya Kaloleni – Kilifi.
Ni timu ambayo inatia fora viwanjani sio tu Kwa mashabiki wake kutoka eneo la Kaloleni bali kuvutia umaarufu kote katika kaunti ya Kilifi.
Kwa sasa timu hiyo inashiriki ligi ya kimaeneo baada ya kushushwa daraja ligi ya divisheni ya pili ukanda wa Pwani kaskazini, chini ya kocha mkuu.
Hivi majuzi timu hiyo ilishiriki katika kombe maalum la CocoFm Super Cup makala ya kwanza yaliyofanyika Jumanne ya Disemba 16 na Jumatano ya Disemba 17 katika uga wa Mmkoroshoni mjini Kilifi ambapo iliibuka na kombe hilo.
Kombe hili ambalo lilidhaminiwa moja Kwa moja na kituo cha utangazaji cha Coco fm Kwa ushirikiano na Wakfu wa George Kithi, linalenga kukuza zaidi talanta kutoka nyanjani haswa timu kama hii ya Mariakani FC.
Kikosi hicho kinchonolewa na Godfrey Gari kilianza mashindano hayo kwa kishindo baada ya kuinyuka klabu ya Interdebaso ya kaunti ndogo ya Kilifi Kaskazini magoli 4-2 kupitia matuta au penalti , baada ya sare ya goli 1-1 muda wa kawaida.
Pia Mariakani waliibuka na ushindi wa 4-3 kupitia matuta au penalty baada ya sare ya magoli 2-2 katika mchezo wa nusu fainali ugani Mkroshoni.rama chengo na issa mwachiwayo
Katika fainali vijana hao walitumia mbinu ile ile ikizamisha meli Beach Bay marufu kama the Worriors of the Bay magoli 4-2 kupitia mikwaju ya matuta baada ya sare tasa muda wa kawaida wakifunga penalty zote.
Penalti zikifungwa na Munga Mwatuya,mwaringa Birya,Rama Chango,Julius Timona.
Mariakani walijishindia shilindi laki 2 kwa kuwa bingwa pamoja na kombe na medali rasmi katika hafla ya kihistoria uwanja ukiwa umefurika.
Kikosi cha Mariakani FC
1 Ayanga kayo
2 Nyawa mrinzi
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.
Sports
Bingwa wa dunia mbio za mitaa 1500 Faith Kipyegon ateuliwa kuwania tuzo za kila mwaka za ‘Laureus World Sportswoman of the Year.’
Nyota wa mbio za masafa ya kati kutoka Kenya, Faith Kipyegon, amepata uteuzi wake wa tatu mfululizo kuwania tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Kike wa Mwaka katika hafla maarufu ya Laureus World Sports Awards, hatua inayozidi kuthibitisha ubabe wake katika kizazi hiki cha wanariadha.
Tuzo hizo, zinazotambuliwa kimataifa kama “Oscars za Michezo”, huandaliwa na Laureus Sport for Good Foundation na hulenga kutambua mafanikio ya kipekee, uthabiti na mchango chanya wa michezo duniani.
Uteuzi wa Kipyegon kwa miaka mitatu mfululizo unaonyesha si tu kipaji chake, bali pia uimara wa kiwango chake cha juu kwa muda mrefu. Mwaka 2024 aliteuliwa baada ya msimu wa kihistoria wa 2023 ambapo alivunja rekodi tatu za dunia na kushinda dhahabu mbili katika Mashindano ya Dunia.
Mwaka 2025 alirejea tena kwenye orodha ya wateule kufuatia mafanikio makubwa katika Michezo ya Olimpiki ya Paris, ambako aliweka historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kushinda medali tatu za dhahabu mfululizo katika mbio za mita 1,500.
Sasa mwaka 2026, anawania tuzo hiyo tena baada ya kuvunja rekodi yake mwenyewe ya dunia ya mita 1,500 na kutwaa taji lake la nne la dunia katika msimu bora wa 2025.
Katika kinyang’anyiro cha mwaka huu, Kipyegon anakutana na ushindani mkali kutoka kwa nyota wengine wa kimataifa akiwemo Sydney McLaughlin-Levrone, Melissa Jefferson-Wooden, Aitana Bonmati, Aryna Sabalenka, na Katie Ledecky.
Uteuzi huu unaendeleza hadhi ya Kipyegon kama mmoja wa wanariadha bora zaidi duniani na fahari kubwa kwa Kenya katika jukwaa la kimataifa.

