Connect with us

Sports

Mary Moraa Amuomba Rais Ruto Kuwatunza Wanariadha Baada ya Mashindano ya Dunia Tokyo 2025

Published

on

Mshindi wa medali ya shaba ya Olimpiki Mary Moraa amemuomba Rais William Ruto aendeleze moyo wake wa ukarimu aliouonyesha kwa wachezaji wa mpira wa miguu, pia kwa nyota wa riadha wa Kenya wanapojitayarisha kwa Mashindano ya Dunia ya Riadha 2025 jijini Tokyo.

Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi, ambako Kiongozi wa Taifa akikabidi bendera kwa kikosi hicho, Moraa aliahidi medali kwa taifa lakini akasisitiza Rais atambue pia kujitolea kwa wanariadha.

Sisi kama timu ya Kenya, tuko tayari kwenda Mashindano ya Dunia, kushinda dunia, na tunakuahidi utarudi na medali kuu. Na wewe kama baba yetu, macho yote yako kwako, tunatumaini utatuunga mkono,” alisema Moraa.

Rais Ruto alitumia hafla hiyo kutangaza nyongeza kubwa ya posho na zawadi kwa wanariadha. Akiagiza Waziri wa Michezo Salim Mvurya kuongeza posho ya kila siku ya wanariadha kutoka dola 60 (Sh7,740) hadi dola 200 (Sh25,800), huku maafisa wakipata dola 300 (Sh38,700).

Mnajua hawa watu; kabla hawajafika hapa, wamepitia jasho mazoezi ya asubuhi na mapema, jioni , na kujitolea katikati yake,” alisema Ruto. “Kwa hivyo maagizo yangu ni kwamba tuongeze malipo yao kutoka dola 60 hadi 200 kwa siku.”

Rais pia alithibitisha kuwa zawadi za medali zimepanda; mshindi wa dhahabu sasa atapokea Sh3 milioni, kutoka Sh750,000 za awali, wakati mshindi wa fedha atachukua Sh2 milioni ukilinganisha na Sh500,000 za awali.

Washindi wa shaba watatunukiwa Sh1 milioni, ongezeko kutoka Sh350,000.

Niliahidi kuwa tutapitia upya zawadi kwa wachezaji wetu wa michezo. Tumelifanya kwa mpira wa miguu na sasa kwenye riadha. Safari hii, mwanariadha yeyote wa Kenya atakayeshinda dhahabu Tokyo ataondoka na Sh3 milioni,” alisisitiza Ruto.

Katika Mashindano ya Dunia ya Riadha ya mwaka 2023 huko Budapest, Kenya iliwasilisha wanariadha 52 wanaume 28 na wanawake 24 na kumaliza katika nafasi ya tano kwa jumla, ikiwa na medali 10 (dhahabu 3, fedha 3, na shaba 4).

Mashindano ya Tokyo yatafanyika kuanzia Septemba 13 hadi 21, yakitarajiwa kuvutia zaidi ya wanariadha 2,000 kutoka mataifa karibu 200. Kenya inalenga kuvunja rekodi yake ya Budapest na kuimarisha nafasi yake ya utawala duniani.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sports

Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting

Published

on

By

Mshambuliaji Kai Havertz aliifungia Arsenal F.C. bao la ushindi katika dakika za mwisho kabisa, na kuisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Sporting CP katika mechi ya mkondo wa kwanza wa robo fainali ya UEFA Champions League iliyochezwa Jana usiku.

Kikosi cha kocha Mikel Arteta kilifika katika Uwanja wa Estadio Jose Alvalade kikiwa kimeathiriwa na vipigo viwili mfululizo dhidi ya Manchester City F.C. kwenye fainali ya Kombe la Ligi na Southampton F.C. katika robo fainali ya Kombe la FA.

Kwa mara nyingine, Arsenal haikucheza kwa kiwango chake bora, lakini ilifanikiwa kupata ushindi kutokana na uokoaji mzuri wa kipa David Raya pamoja na umakini wa Havertz aliyefunga bao la ushindi katika muda wa nyongeza.

Arsenal sasa ina nafasi kubwa ya kufuzu nusu fainali kabla ya mechi ya marudiano itakayochezwa kaskazini mwa London tarehe 15 Aprili, ingawa italazimika kuboresha kiwango chake ikiwa inataka kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza.

Vipigo dhidi ya City na Southampton vilikuwa mara ya kwanza msimu huu kwa Arsenal kupoteza mechi mbili mfululizo, huku kipigo cha Kombe la FA kikiwa cha tano kwao msimu huu.

Athari za matokeo hayo bado zilionekana Lisbon, ambapo Arsenal ilipata ugumu wa kucheza kwa mwendelezo mzuri, lakini kama ilivyokuwa mara kadhaa msimu huu, walipata njia ya kushinda licha ya kutocheza vizuri.

katika mechi nyingine hatua ya robo fainali ni kwamba Bayern Munich waliondoka na ushindi wa magoli 2-1 mikononi mwa Real Madrid katika uwanja wao wa nyumbani Estadio Santiago Bernabeu.

Magoli ya Bayern yakitiwa kimyani na mshmabulizi Luis kipindi cha kwanza naye Erling Haaland kipindi cha pili.

Mechi ya marudiano itachezwa juma lijalo April 15.

Continue Reading

Sports

Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)

Published

on

By

Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.

Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.

SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

Continue Reading

Trending