Sports
Rasmi Mshambulizi wa Uswidi Alexander Sasa ni Mali ya Liverpool
Kilabu ya Liverpool wakubaliana kumsajili mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak kutoka Newcastle United
Liverpool wamekubaliana kumsajili mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak kutoka Newcastle United kwa mkataba wa muda mrefu kwa ada ya rekodi ya Uingereza inayokadiriwa kufikia pauni milioni 130 ($175 milioni), vyombo vya habari vya Sky Sports News na The Athletic viliripoti Jumapili.
Mazungumzo ya muda mrefu kuhusu dili hilo yamekuwa yakitawala dirisha la usajili la Ligi Kuu ya England, ambalo linahitimishwa Jumatatu, huku ofa ya awali ya Liverpool ya pauni milioni 110 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ikikataliwa mapema Agosti.
Mchezaji huyo amepasi vipimo vya kimatibabu na anatarajiwa kumwaga wino mkataba wa miaka mitano na The Reds.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

