Sports
Sancho Kurejea Manchester United.
Kilabu ya Chelsea imelipa ada ya pauni milioni 5 na kuvunja mkataba kati yao na winga wa Manchseter United Jadon Sancho ambaye amekuwepo kilabuni humo japo kwa mkopo.
The Blues walikua tayari kulipa ada ya pauni milioni 25 kwa Mashetani Wekundu kupata sahihi ya winga huyo ila matakwa ya binafsi ya mchezaji huyo ikiwemo mshahara wake wa kila wiki ilizua kutoelewana na badaye kilabu hiyo kubaki na si lingine ila kuvunja mkataba huo.
Sancho mwenye umri wa miaka 26 amekua na wakati mzuri ugani Stamford Bridge akisaidia Chelsea kumaliza ndaani ya nne bora Epl na kushinda kombe la Europa Conference Ligi baada ya kuwa na wakati mgumu Manchester akishindwa kutamba chini ya kocha Erik Ten Hag na badaye Ruben Amorim.
Kinachosubiriwa kuona iwapo atarejea katika kambi ya Manchester ama atasaka makao kwingineko msimu ujao.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

