Sports
Senegal Wako Tayari Kutetea Ubingwa Asema Kocha Diallo
SENEGAL-Wanajiita The Lions of Teranga kwa jina la Utani.
Ni mabingwa watetezi wa kombe la CHAN wakishinda kombe hilo na lao la pekee mwaka 2022 mjini Algiers Aljeria.
Kocha mkuu wa kikosi hicho ni Pape Thiaw ila majukumu ya kipute cha CHAN yamepewa aliyekua mchezaji wa taifa hilo Souleymane Diallo kuongoza vijana hao akiwa pia amenoa kikosi cha vijana chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20.
mkufunzi huyo amesema lengo lao kuu ni kutetea ubingwa wa taji hilo kwani wana kikosi bora na wamejipanga vilivyo.
“Sisi ni mabingwa na tunakuja kutetea ubingwa wetu katika kombe la CHAN mwaka huu tuna kikosi chipukizi na nina amini wako tayari kwa changamoto yoyote ile.”
Vijana hao waliadhibu Taifa la Liberia magoli 3-0 nyumbani kabila ya kutoka sare ya goli 1-1 mechi ya marudio na kujikatia tiketi hiyo.
Wachezaji nyota wakuangaziwa katika kikosi cha The Lions of Teranga ni pamoja na mshambulizi Oumar Bar anayekipiga na kilabu ya US Goree ya taifa hilo mwingine ni kiungo Baye Assane Ciss miongoni mwa wengine.
Timu hiyo inajivunia nyota Lamine Camara ambaye alingaa mwaka 2022 na sasa anapiga na Monaco ya Ufaransa baada ya kupata ufanisi mkubwa.
Senegal wako kundi D pamoja na mataifa ya Congo,Sudan na Nigeria.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

