Sports
Stars Kambini Kwa Maandalizi Ya CHAN
Timu ya Taifa ya soka Harambee Stars kimeingia kambini tayari kwa maandalizi ya Chan mwezi ujao katika mataifa ya Kenya,Uganda na Tanzania.
Vijana wa Nyumbani wamekaribishwa kambini na Waziri wa michezo Salim Mvurya na katibu mkuu Elija Mwangi na,rais wa Shirikisho la soka FKF Hussein Mohammed.
Stars itaendeleza mazoezi ugani Ulinzi Sports Complex chini ya kocha mkuu Benni MacCarthy ambaye amesema kwamba wako katika hali shwari,alipoulizwa kuhusu wachezaji wengine kukosana kikosini mwalimu huyo amedai kwamba hawezi akafurahisha kila mmoja wakati wa Uteuzi.
“Huwezi kumpendeza kila mtu,Sijakuja kufurahisha kila mtu ila malengo yake ni kuteua kikosi bora kwa ajili ya Taifa,Ni mimi ndiye kocha na nimetazama hawa wachezaji kwa hivyo lengo ni kunoa stars kuleta matokeo chanya timuni.”
Stars watakua kambini kabila ya kuelekea Tanzania kwa taji la CECAFA mataifa manne ;Kenya, Uganda,Tanzania na Sudan Kusini.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

