Sports
Timu Za Kenya Mpira Wa Hoki Zajianda Mechi Za Bara Afrika
Timu za Kenya upande wa akina dada na wanaume mpira wa Hoki zimezidi kujitia makali ugani City Park Nairobi tayari kwa mashindano ya Kombe la Bara Afrika mjini Ismaella Misri Oktoba 11-18.
Vikosi vyote vimakua na zaidi ya mazoezi ya mara tatu kwa siku wakilenga kuandikisha matokeo ya kuridhisha katika makala ya mwaka huu.
Kulingana na kocha wa Akina dada Meshack Senge wanajinoa zaidi ili kuboresha matokeo walioandikisha mwaka 2022 mjini Accra Ghana.
Katika makala ya mwaka 2022 katika Taifa la Ghana Kenya ilijinyakulia taji la Shaba kwa akina dada huku wenyeji Ghana wakimaliza nafasi ya Tatu nayo Misri nafasi ya kwanza na kushinda Dhahabu.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

