Sports
Tottenham Yamfuta Kazi Kocha Postecoglou
Kilabu ya Tottenham Hotspurs ya London Kaskazini imetangaza kumfuta kazi kocha wake Ange Poetecoglou siku cheche tu baada ya mwalimu huyo kuongoza kilabu yake kuvunja ukimya wa miaka 17 na kutua taji la UEFA Europa Ligi kwa kushinda Manchester United goli 1-0 ugani San Mames Uhispania Mei 21.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari kilabu hiyo kupitia kwa mwenyekiti wake Daniel Levy imesema kwamba imeweza kupiga msasa utenda kazi wa kocha huyo katika msimu mzima na hivyo basi kukubaliana kumuonyesha mlango raia huyo wa Australia.
Spurs walimaliza nafasi ya 17 jedwali la Ligi ya Uingereza na alama 38 na matokeo hayo huenda yamechangia kufurusha kwa mwalimu huyo kocha huyo akipoteza mechi 21.
Postecoglou si wa kwanza kufutwa kazi na spurs katika njia tatanishi wengine ni kocha Jose Mourinho,Nuno Espirito Dos Santos na Mauricio Pochettino.
Hata hivyo taarifa hiyo haijachukulia vyema na baadhi ya wachezaji ambao wameshutuliwa na taarifa hiyo baada ya ufanisi wa kocha huyo Spurs.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

