Sports
Uganda Cranes Yaangukia Pabaya Katika Mchezo wa Ufunguzi wa CHAN
Timu ya taifa ya Uganda Cranes yaanza vibaya kipute cha CHAN baada ya kutiwa darasani, kabila ya kuchabangwa magoli 3-0 na The Desert foxes mechi ya ufunguzi ugani Nelson Mandela Stadium mjini Kampala hapo jana.
Wageni walichukua uongozi wa mapema kupitia mshambulizi Ayoub Ghezela dakika ya 36 kabila kuongeza goli la pili dakika ya 76 kipindi cha pili kupitia mshambulizi wa CR Belouzidad Abderahmene Meziane kabila ya Sofiane Bayazid kufunga la tatu dakika tatu badaye,na kuzamisha meli la Cranes ambao walikua wameahidiwa donge nono pesa milioni 43 kwa kila ushindi na Rais Yoweri Museveni.
Katika mechi nyingine;Guinea walianza vema kwa kunyuka Niger goli 1-0 katika uwanja huo uo.
Katika ratiba ya leo ni kwamba mabingwa watetezi Senegal ‘The Lions Of Teranga’watamenyana na ‘The Super Eagles’ Ya Nigeria saa mbili usiku ugani Amaan Complex Zanzibar.
Mechi ya kwanza itahusisha Congo dhidi ya Sudan saa kumi na mbili jioni.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

