Sports
US Open: Jannik Sinner aingia raundi ya tatu, Wong aandika historia kwa Hong Kong
Bingwa mtetezi wa wanaume mpira wa tenesi Jannik Sinner aliingia raundi ya tatu ya US Open hapo jana huku Coco Gauff na Iga Swiatek wakipambana kuendeleza ndoto zao za kutwaa ubingwa.
Sinner alimfagia Mwaustralia Alexei Popyrin kwa seti 6-3, 6-2, 6-2 na kuongeza rekodi yake ya ushindi katika michuano ya Grand Slam kwenye uwanja mgumu hadi mechi 23 mfululizo.
Mchezaji huyo namba moja kwa kupanda viwango kutoka Italia ameanza kwa kishindo katika azma yake ya kuwa mwanaume wa kwanza kutetea taji la US Open tangu Roger Federer aliposhinda mara tano mfululizo kati ya 2004–2008.
“Ninalenga kuboresha huduma (serve), lakini mengine najihisi vizuri,” alisema Sinner.
Sasa Sinner atakutana na mchezaji wa Kanada namba 27 kwa viwango, Denis Shapovalov, katika raundi ya tatu siku ya Jumamosi.
Tayari amefika fainali ya Grand Slam zote tatu msimu huu, akitwaa Australian Open na Wimbledon, huku akikubali kichapo kutoka kwa Carlos Alcaraz kwenye French Open.
Mshindi namba tatu kwa viwango bora Alexander Zverev alishinda kirahisi 6-4, 6-4, 6-4 dhidi ya Mbritania Jacob Fearnley, huku Lorenzo Musetti akimnyamazisha Mbelgiji David Goffin.
Mchezaji namba 15 kwa viwango kutoka Urusi Andrey Rublev alimshinda Tristan Boyer wa Marekani (wild card) kwa seti nne, na sasa ataumana na kijana wa Hong Kong Coleman Wong katika hatua ya 32 bora.
Wong, mwenye umri wa miaka 21 na aliyefuzu kupitia mashindano ya awali, aliendeleza hadithi yake ya kusisimua New York kwa kumshinda Mwaustralia Adam Walton 7-6 (7/5), 6-2, 4-6, 6-4.
Wong, anayerankiwa namba 173 duniani, tayari aliweka historia mapema wiki hii kwa kuwa mwanaume wa kwanza kutoka Hong Kong kushinda mechi ya Grand Slam ya mchuano wa mtu mmoja.
“Hii ni ndoto yangu, kitu ambacho kila mchezaji wa tenisi huota — kuendelea kupiga hatua kwenye Slam,” alisema Wong.
Katika mechi ya mwisho ya siku, Mmarekani mchezaji namba 14 Tommy Paul hatimaye alimshinda Mreno Nuno Borges saa 7:46 usiku katika pambano la seti tano kali.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

