Sports
Wanariadha wa Wakenya kuwinda nishani kwenye fainali mbili leo Tokyo,Japan
Wanariadha wa humu nchini watalenga kujiongezea nishani zaidi katika siku ya tano ya mashindano ya Riadha Duniani mjini Tokyo Japan leo jioni.
Mshindi wa nishani ya shaba ya dunia mwaka 2023 Faith Cherotich atashiriki fainali ya mita 3000 kuruka viunzi na maji kuanzia saa tisa na dakika 57 alasiri, akilenga kutwaa dhahabu ambayo ilinyakuliwa na Wakenya kwa mara ya mwisho mwaka 2019.
Cherotich aliye na umri wa miaka 21 atashirikiana na Doris Lemngole kwenye fainali hiyo huku upinzani ukitarajiwa kutoka kwa Mkenya anayekimbilia Bahrain Winfred Yavi na bingwa wa Olimpiki mwaka 2020 Peruth Chemtai.
Baadaye saa kumi na dakika 20 bingwa wa Dunia mwaka 2019 Timothy Cheruiyot na bingwa wa zamani wa Dunia kwa chipukizi Raynold Cheruiyot watatimka fainali ya mita 1500.
Kenya ni ya pili kwenye msimamo wa medali baada ya siku nne za mashindano hayo ikiwa na medali 5 ,dhahabu 3 fedha 1 na shaba 1.
Marekani inaongoza kwa dhahabu 6 na shaba 2.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

