Sports
Chebet atwaa dhahabu,Kipyegon fedha mashindano ya Riadha Duniani Jumamosi
Mkenya Beatrice Chebet aliongoza Kenya kunyakua nishani za dahahbu na fedha katika fainali ya mita 5000 katika siku ya nane ya mashindano ya Riadha Duniani Jumamosi alasiri.
Chebet ambaye pia alikuwa ameshinda dhahabu ya mita 10,000 ,ameziparakasa mbio za mbio za mita 5,000 kwa kutumia muda wa dakika 14:54.36.
Bingwa wa dunia wa mita 1500 Faith Kipyegon ameshinda nishani ya fedha kwa dakika 14:55.07, wakati Nadia Batocletti wa Italia akiridhia sahaba kwa muda wa dakika 14:55.42.
Chebet ndiye Mkenya wa pili tangu Vivian Cheruiyot aliponyakua dhahabu za mita 5000 na 10,000 mwaka 2011 mjini Daegu, Korea.
Aidha Chebet anashikilia rekodi za Dunia za mbio za mita 5,000 na 10,000 na kilomita 5.
Kenya ni ya pili kwenye msimamo wa medali kwa nishani 5 za dhahabu, 2 za fedha na 2 za shaba.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

