Sports
Harambee Starlets Kuelekea TZ Kwa Mechi Za CECAFA
Kikosi cha soka akina dada humu nchini Harambee Starlets kimeondoka mapema leo kuelekea mjini Dar es Salaam Tanzania kwa mashindano ya CECAFA baina ya mataifa Afrika ya Mashriki.
Vipusa hao chini ya kocha Beldine Odemba ilifanya mazoezi mepesi hapo jana kabila ya kukwea pipa hii leo wachezaji 23 wakisafiri ikiwa ni wachezaji wa kimataifa na wanaocheza ligi ya nyumbani.
Starlets wanafungua kampeini Jumapili dhidi ya Burundi kabila ya kumenyana na Uganda ,Sudan Kusini na badaye kumaliza na wenyeji Tanzania.
Kwa mujibu wa kocha Beldine ni kwamba amekichagua kikosi chenye ubora huku badhi ya majina makubwa yakikosekana akiwemo mshmabulizi wa Simba Queens Jentrix Shikangwa,Teresah Engesha pamoja na Mwanahalima Dogo wote wanakosekana kwenye kambi hiyo ya Starlets.
Mechi zote zinapigwa katika uwanja wa Azam Sports Complex mjini Dar es Salaam.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

