Sports
Harambee Stars Kuvaana Na Chad Mechi Ya Kirafiki.
Timu ya Taifa Harambee Stars chini ya kocha Benni Mccarthy kushuka dimbani majira saa kumi jioni Ugani Stade de Marrakech Morocco ikiwa ni mechi ya kirafiki.
Kwa mujibu wa mwalimu wa Stars Mccarthy mechi hizi ni muhimu kujenga kikosi kwa majukumu ya siku za usoni lakini pia kwa taji la Chan sawa na Afcon mwaka 2027.
“Ni muda mzuri mimi kufahamu vijana wangu na kuanza kuanda timu yenye ubora kwa minajili ya siku za usoni na wachezaji wa nyumabani watasaidia sana CHAN mwezi Agosti.”
Baada ya mechi hiyo Stars watacheza mechi nyingine na taifa hilo Juni 10.
Rais wa Fkf Hussein Mohammed amekariri kikosi hicho kitaelekea Uarabuni kwa maozezi kabambe kabila ya Chan humu nchini.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

