Sports
Kevin De Bruyne Atua Napoli
Ni rasmi kilabu ya Napoli imetangaza kupata sahihi ya kiungo wa zamani wa Manchester City Kevin De Bruyne raia wa Ubelgiji.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 amewaga wino kwenye karatasi kandarasi ya miaka miwili na mabingwa hao wa Serie A.
Kupitia kwenye tuvuti ya kilabu hiyo Rais Aureli De Laurenttis ameweza kuthibitisha kuwasili kwa nyota huyo ambaye aliwika sana ligi kuu uingereza akishinda kila kitu na Mancity kwa kumwambia ‘KARIBU NAPLES’.
Kiungo huyo mbunifu alitangaza kuondoka City baada ya kuwajibikia kilabu hiyo kwa muda miaka minane akishinda mataji sita ligi ya EPL ,Moja kilabu bingwa ulaya,manne ya FA na mataji mengine.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

