Sports
Kikosi cha Voliboli Malkia Strikers Waondolewa FIVB World Championships
Timu ya taifa ya wanawake ya voliboli ya Kenya, Malkia Strikers, imeondolewa kwenye mbio za ubingwa wa dunia wa FIVB baada ya kupoteza kwa ushindani kwa seti 1-3 (17-25, 25-15, 15-25, 14-25) dhidi ya Poland katika uwanja wa Saphan Hin wenye uwezo wa kuketi mashabiki 4000 huko Phuket, Thailand.
Kenya ilishinda seti moja katika mchezo huo, ikiwa ni hatua makubwa ikilinganishwa na mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Ujerumani.
Jumamosi, Kenya ilipoteza kwa seti 3-0 dhidi ya Ujerumani katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi “G”.
Kenya na Vietnam, ambazo hazijapata ushindi wowote kwenye mashindano haya, zitamenyana Jumatano saa 7 mchana saa za Afrika Mashariki katika mchezo usio na maana ya kufuzu.
Ujerumani na Poland, ambao tayari wamefuzu kwa raundi ya pili baada ya kushinda mechi mbili za makundi, watakutana Jumatano saa 10:30 jioni saa za Afrika Mashariki kuamua nani atamaliza kileleni mwa kundi.
Kocha wa Kenya, Geoffrey Omondi, alisema hakuridhishwa na matokeo ya Jumatatu, akibainisha kuwa sasa hawana budi kushinda mechi iliyosalia.
“Kushinda seti moja dhidi ya timu ya tatu bora duniani ni jambo la kujivunia, lakini nilitamani matokeo bora zaidi. Nilihitaji kushinda seti ya nne ili kulazimisha seti ya tano, na huenda tungeibuka washindi, lakini haikuwa hivyo. Kwa sasa angalau tuna siku ya kesho ya kupumzika na kujiandaa kwa mchezo dhidi ya Vietnam Jumatano,” alisema Omondi.
“Vietnam wanacheza kwa kasi, kwa hivyo tunahitaji kuwa katika kiwango chetu bora tukitaka kuwashinda. Kumekuwa na maendeleo makubwa kutoka kwa timu—ubora wa mtu mmoja mmoja, ushirikiano na maelewano—na tunahitaji tu kuendeleza hayo katika mchezo ujao. Tulipoteza dhidi ya Vietnam kwenye mechi za kirafiki, lakini tunatarajia kulipa kisasi,” aliongeza.
Kocha wa Poland, Stefano Lavarini, alikiri kuwa Kenya iliwasumbua sana.
“Kama nilivyosema kwenye mahojiano ya awali kwamba Kenya si timu ya kubezwa, na tulipata uthibitisho leo. Tulipata changamoto muda wote wa mchezo, lakini ninafurahi tuliweza kuwadhibiti na kushinda. Ni timu yenye nguvu za mwili ambayo inaweza kutoa mshangao,” alisema Lavarini.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

