Sports
Kilabu ya Chelsea Ndiyo Mabingwa wa Conference League
Kilabu ya Chelsea ya Uingereza imekua ya kwanza kushinda taji la Kilabu Bingwa Ulaya,taji la Uefa Europa ligi,Uefa Supa Cup na Taji la Conference ligi katika historia ya mataji hayo barani Ulaya.
Hii ni baada ya The Blues kutia darasani kabla ya kuchachafya kilabu ya Real Betis ya Uhispania kichapo cha magoli 4-1 uwanjani majeski stadium,Poland fainali ya conference ligi.
Kilabu ya Real Betis walitanguliwa kufunga kupitia winga matata wa taifa la Morocco Abde Elizouzoli dakika ya 9 Lakini chelsea walikua na jambo lao wakirejea kwa kishindo kipindo cha pili kupitia magoli ya kiungo MuArgentina Enzo Fernandez dakika 65,kisha Mshambulizi wa taifa la Senegal Nicholas Jackson akipachika wavuni goli la pili dakika ya 70,
winga matata wa Manchester United Muingereza Jadon Sancho aliongeza la tatu dakika ya 70,huku Kiungo mkabaji Moses Caicedo akizika Betis kwa chuma cha nne kunako dakika ya 93 na kunyakua kombe hilo.
Kombe hilo ni taji la kwanza kwa kocha Enzo Maresca kilabuni humo na hakuficha furaha yake baada ya kuwapa furaha mashabiki wa The Blues.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

