Sports
Kipa wa Manchester United, Andre Onana, Akamilisha Uhamisho wa Mkopo wa Msimu Mzima Trabzonspor
Kipa wa kilabu ya Manchester United kutoka Cameroon, Andre Onana, amekamilisha uhamisho wa mkopo wa msimu mzima kuelekea klabu ya Uturuki, Trabzonspor.
Mustakabali wa Onana katika Old Trafford ulikuwa na wasiwasi baada ya United kumsajili kipa wa Antwerp, Senne Lammens, kwa euro milioni 21 (£18.2 milioni) pamoja na nyongeza.
Onana mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na United akitokea Inter Milan mwaka 2023 kwa ada ya awali ya euro milioni 51 pamoja na nyongeza ya hadi euro milioni nne, na akamaliza msimu wake wa kwanza na medali ya ubingwa wa FA Cup.
Hata hivyo, jeraha la misuli ya paja lilimzuia kushiriki na kikosi wakati wa maandalizi ya msimu, na akafanya kosa katika mchezo wake wa kwanza wa msimu mpya wakati United iliposhushwa hadhi baada ya kutolewa na Grimsby kwenye Carabao Cup.
Kufika kwa Lammens kulikuwa pigo la mwisho kwa Onana.
“Kipa wa Manchester United, Andre Onana, amejiunga na Trabzonspor kwa mkopo kwa kipindi chote cha msimu wa 2025/26, kutegemea kibali cha kimataifa na usajili,” United walithibitisha kupitia taarifa rasmi.
“Uhamisho huu umekamilika kabla ya dirisha la usajili la Uturuki kufungwa siku ya Ijumaa. Tunamtakia Andre mafanikio,” taarifa hiyo ya klabu iliongeza.
United watarudi uwanjani baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa kwa mchezo wa ugenini dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Manchester City, siku ya Jumapili.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

