Sports
Kocha Wa Gor Zico Ataka Mashemeji Derby zichezwa Nje ya Nairobi
Mkufunzi mshikilizi wa kilabu ya Gor Mahia Zedekiah Zico Otieno amesema kwamba ni wakati mwafaka kwa mechi nyingi za debi la Mashemeji kati mahasimu wa tangu jadi Gor na Afc Leopards zichezwe nje ya mji wa Nairobi.
Mwalimu huyo aliysema hayo kwenye kikao na wanahabari ambapo amesema kwamba itakua ni raha kuona mechi hiyo ikichezwa Kakamega,Mumias au hata Busia miaka zijazo.
Hayo yanajiri huku Zico akiweka wazi wanakwenda uwanjani Raila Odinga katika kaunti ya Homabay kusaka alama tatu muhimu siku ya jumatano dhidi ya Afc Leopards.
“Nadhani itakua ni mechi mgumu kwani debi haijakua rahisi ila tunakwenda kusaka alama tatu muhimu na kupunguza mwanya kati yetu na wapinzani wetu,ndaani ya Kogalo tunajua ushindi tu na najua mashabiki wanataka hilo,lengo letu ni ushindi tu siku ya Jumatatu.”
Tiketi za mchuano huo zinauzwa kwa shilingi 300 mshabiki wa kawaida huku mashabiki mashuhuri wakilipia shilingi 3000.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

