Sports
Kocha Wa Starlets Odemba ajiuzulu
Mkufunzi wa timu ya taifa soka akina dada Harambee Starlets Beldine Odemba ametangaza kujizulu wadhifa wake kama kocha mkuu wa kikosi hicho baada ya kichapo cha magoli 5-1 na Morocco mechi ya kirafiki.
Kwa mujibu wa mwalimu huyo kilichomfanya kuondoka katika kambi ya timu hiyo ni kukosa ungwaji mkono katika kazi yake ya kunoa starlets akiondoka siku chache tuu kabla ya kungoa nanga kwa taji Cecafa nchini Tanzania Juni 12.
Mkufunzi huyo ambaye ameshinda ligi ya akina dada na kilabu ya Kenya Bullets amedokeza kwamba ni swala ambalo ameliwazia kwa muda na kwa sasa anaelekeza nguvu zote kwa kikosi hicho taji la Cecafa baina ya vilabu.
Ripoti zinaarifu kwamba kocha wa Kibera Soccer Women David Vijago atatangazwa kocha mpya wa Starlets akisaidiana na Alex Alumira ambaye amewahi kuwa kocha wa timu hiyo.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

