Sports
Manchester United Yamsajili Cunha
Kilabu ya Manchester United imekamilisha usajili wa kiungo mshambulizi wa kilabu ya Wolves Matheus Cunha raia wa Brazil.
Kupitia kwenye tuvuti ya kilabu hiyo imetangaza kukubaliana na Wolves pamoja na matakwa ya kibinafsi ya mchezaji huyo
The Red Devils wametumia kitita cha pauni milioni 62.5 kunasa mchezaji huyo mwneye umri wa miaka 26.
Mshambulizi huyo atawasili kwa vipimo vya kimatibabu ugani Carringhton hapo kesho na tangazwa rasmi kuwa sajili wa kwanza kwa kocha mkuu Ruben Amorim.
Kwa mujibu wa nguli wa taarifa za Uhamisho Barani Ulaya Fabrizio Romano Cunha alitaka United pekee wala si kilabu yoyote ile licha kuvutia vilabu mbalimbali barani ulaya.
Mbrazil huyo anatarajiwa kutia wino mkataba wa miaka mitano uwanjani Old huku United wakiaminika sasa kuzamia kupata mshambuliz wakiwinda mshambulizi Victor Osimhen wa taifa la Nigeria na Victor Gyokeres wa taifa la Sweeden.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

