Sports
Mancity Waingia Kwenye Hatua Muondoano Kombe La Dunia
Kilabu ya Manchester City imejiunga na mibabe katika raundi ya 16 bora kombe la Dunia baina ya Vilabu nchini Marekani.
Hii ni baada ya vijana wa kocha Pep Guardiola kufumua Juventus ya Italia magoli 5-2 uwanjani Camping World Stadium,winga matata Jeremy Doku aliwatanguliza City dakika ya 9 kabila ya Juve kujibu kupitia kwa kiungo Teun Koopmeiners dakika ya 26 kupitia kwa Piere Kalulu naye mshmabulizi Erling Haaland akiweka la tatu dakika ya 52.
Kiungo Phil Foden aliweka kambani chuma cha nne dakika 67 naye Savinho akifunga la tano.
Katika Droo timu 16 bora ni kwamba ;Inter vs Fluminese,Mancity vs Al-Hilal,Real vs Juventus
Jumamosi;
Palmeiras vs Botafogo fc saa moja usiku 7;00pm
Chelsea vs Benfica saa tano usiku 23;00pm
Jumapili:
Psg vs Inter Miami 7;00pm
Flamengo vs Bayern Munich 23:00pm
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

