Sports
Mkenya Faith Kipyegon aishindia Kenya dhahabu ya Dunia ya Tatu katika mita 1500
Bingwa wa Olimpiki Faith Kipyegon amenyakua nishani ya nne ya dhahabu ya dunia katika mbio za mita 1500 na ya tatu mtawalia leo jioni mjini Tokyo, Japan.
Kipyegon ameziparakasa mbio hizo kwa muda wa dakika 3 sekunde 52.15, huku Dorcas Ewoi aliyekuwa akishiriki mashindano ya Dunia kwa mara ya kwanza akinyakua fedha kwa dakika 3 sekunde 54.94.
Jessica Hull wa Australia ameshinda shaba kwa muda wa dakika 3 sekunde 55.15, naye Nelly Chepchirchir wa Kenya akaridhia nafasi ya nne.
Bingwa huyo mara tatu wa Olimpiki ndiye mwanariadha wa kwanza kunyakua dhahabu nne za dunia mwaka 2017, 2022, 2023 na mwaka huu.
Kenya ingali ya pili kwenye msimamo wa dunia baada ya kuzoa dhahabu 3, fedha 1 na shaba 1.
Marekani inaongoza msimamo wa dunia kwa dhahabu 6 na shaba 2.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

