Sports
Ojwang Arejea Morans Kwa Msururu Wa Dubai
Naibu kocha wa Shujaa Louis Kisia amemtaja winga wa kilabu ya Nakuru Rfc Chrisant Ojwang wakati wa kukitaja kikosi cha Morans kwa ajili ya mashindano ya dunia ya HSBC World Rugby Sevens Series mjini Dubai.
Mchezaji huyo amekua nje kwa zaidi ya miezi saba baada ya kupata jeraha baya la goti ila kwa sasa amepona na yuko tayari kuwakilisha taifa kibarua yake ya kwanza ni kuongoza Kenya kwneye mashindano ya bara Afrika Juni 21-22 nchini Mauritius.
Wachezaji wengine ambayo wametajwa na kocha huyo ni pamoja na Jackson Siketa,Philip Okeya,Felix Okoth,Javan Otieno na Matoka Matoka.
kikosi hicho kiko kundi A pamoja na Uganda, Ivory Coast na Ghana.
Kundi B kinajumuishwa ,Afrika Kusini,Burkina Faso,Nigeria na Zambia.
Kundi C kinajumisha wenyeji Mauritius,Madagascar,Tunisia na Zimbabwe.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

