Sports
Rais Atoa Ahadi Nono Kwa Stars Kuelekea Mechi Ya Jumapili
Rais William Ruto ametangaza kuwa kila mchezaji wa timu ya taifa atapokea shilingi milioni 2.5 kama marupurupu endapo wataibuka na ushindi kwenye mechi ya mwisho dhidi ya Zambia, Jumapili hii. Hii ni ongezeko la shilingi milioni 1.5 kutoka kiwango cha awali.
Rais alitoa ahadi hiyo alipowatembelea wachezaji katika hoteli yao jijini Nairobi, na kuongeza kuwa kila mchezaji atapewa shilingi milioni 1 watakapofika robo fainali, pamoja na nyumba ya vyumba viwili katika mradi wa nyumba za bei nafuu, popote watakapochagua.
Ahadi hizi zinakuja kufuatia ushindi muhimu wa goli 1–0 uliopatikana jana dhidi ya Morocco katika mechi ya tatu ya michuano ya Kombe la CHAN iliyochezwa Uwanja wa Kasarani.
Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na mshambulizi wa klabu ya Tusker FC, Ryan Wesley Ogam, katika dakika ya 41 ya kipindi cha kwanza, na kuifanya timu ya taifa kuongoza Kundi A kwa alama 7 baada ya mechi tatu.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

