Sports
Rasmi Ronaldo Asaini Mkataba Mpya Wa Miaka 2 Al-Nassr
Mshambulizi nyota wa Taifa la Ureno Cristiano Ronaldo amwaga wino mkataba wa miaka 2 na kilabu yake ya Al Nassr na kupuzilia mbali uvumi kuondoka kwa kilabu hiyo ambayo alijiunga nao msimu wa mwaka 2023 akitokea Manchester United ya Uingereza.
Duru zakuaminika zasema kwamba gwiji huyo atakua anapokea mshahara wa pauni milioni 492 kila mwaka katika kandarasi hiyo nono ambaye imetiwa rasmi sahihi leo.
Mchezaji huyo bora mara tano ulimwenguni, mwenye umri wa miaka 40 atakua anapokea mshahara wa pauni laki 488000 kwa siku na pauni milioni 4 za usafiri ya jeti sawa na pauni asilimia milioni 25 kama marupurupu za sajili.
Vilbu vya Al-Hilal na Intermiami vimekua vikimmezea mate mchezaji huyo mshindi wa kombe la Uefa Nations Ligi na Taifa lake mwezi huu.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

