Sports
Starlets Yaanza Vema CECAFA
Kikosi cha soka akina dada Harambee Starles imeanza vema mashindano ya ukanda wa Afrika Mashriki na kati CECAFA ambayo yanandelea mjini Dar es Salaam Tanzania.
Hii ni baada ya vipusa hao chini ya kocha Beldine odemba kufunga Burundi magoli 3-0 ugani Azam Sports Complex,kiungo wa Vihiga Queens Martha Amunyolet alikua nyota wa mchezaji huyo baada ya kucheka na nyavu mara 2 goli la kwanza dakika 2 na lingine dakika 5 kabila ya mshambulizi wa Kibera Soccer Women Faith Mboya kufunga la tatu dakika 91.
Kikosi hicho kinashuka dimbani dhidi ya Crested Cranes Ya Uganda katika mechi ya pili.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

